Thursday, January 12, 2017

JWTZ yatua UDSM kujenga ‘fensi’ ya mabweni

 

By Kelvin Matandiko, Mwananchi kmatandiko@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mradi wa kujenga uzio wa mabweni mapya 20 ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jirani na Mlimani City, uko chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mkandala amesema hayo wakati akitoa akipokea Sh497 milioni kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ili kufanikisha ujenzi huo ndani ya mwaka mmoja.

Profesa Mukandala amesema ujenzi wa mabweni chini Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) tayari umekamilika kwa asilimia 90.

Ujenzi huo uliwekwa msingi  Oktoba, 2015 na Rais John Magufuli ambapo mabweni hayo yana uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,840 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa maktaba ya kisasa ya chuoni hapo.

“Ujenzi umeshaanza na Jeshi la Wananchi ndiyo wanajenga uzio huo, tena kwa kasi, manufaa ya uzio ni mengi ...maeneo yale yanatumika kama vijiwe, njia za mkato, kuna viwanja michezo, ni karibu na kituo cha mabasi ya abiria. Kwa hiyo itaongeza usalama wa wanafunzi,” amesema Profesa Mkandala.

-->