Majaliwa akerwa na wingi wa mabango kwenye mikutano ya viongozi wakuu
Mirerani.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema wingi wa mabango katika mikutano ya hadhara ya viongozi wakuu ni ishara ya wazi kuwa watendaji wa halmashauri hawawatembelei wananchi na kutatua kero zao.
Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mikutano wa Mererani mkoani Manyara jana jioni, Majaliwa alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro na watendaji wake kukusanya mabango yaliyokuwa yakionyeshwa na wananchi kwani mengi ya matatizo yanapaswa kumalizwa na viongozi hao na aliwaagiza kurejea Mererani siku inayofuata ili waitishe mkutano na kujibu bango moja baada ya jingine.