Wanaofanya uchimbaji Msitu wa Shengena watakiwa kufuata taratibu

Muktasari:

Akijibu swali hilo bungeni leo(Jumatano) Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani, amesema kuwa mtu au taasisi itakayohitaji kufanya shughuli za uchimbaji ndani ya hifadhi hiyo atatakiwa kufuata taratibu za kisheria.

Dodoma. Mbunge wa Same Mashariki (Chadema) Naghenjwa Kaboyoka amehoji juu ya athari za kimazingira zinazotokana na uchimbaji wa madini ya Bauxite unaoendelea katika Msitu wa Shengena.

Akijibu swali hilo bungeni leo(Jumatano) Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani, amesema kuwa mtu au taasisi itakayohitaji kufanya shughuli za uchimbaji ndani ya hifadhi hiyo atatakiwa kufuata taratibu za kisheria.

Amesema taratibu hizo ni zile zitakazozingatia masuala muhimu ikiwamo kufanyika kwa Tathmini ya Athari za Mazingira (TAM) kabla ya kuanza kwa uchimbaji.

Hata hivyo amesema hadi sasa hakuna taarifa rasmi kuhusu uchimbaji wa madini ya Bauxite katika Hifadhi ya Shengena.