Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro aongoza kupokea wanafunzi wa Lucky Vicent

Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro  Anna Mghwira amewaongoza wakazi wa mkoa huo kuwapokea wanafunzi watatu wa shule ya Lucky Vincent waliowasili asubuhi hii kutoka Marekani.

Wanafunzi waliorejea ni Doreen mshana,Sadia Awadh na Wilson Tarimo

Wanafunzi hao walianza kushuka mmoja mmoja kutoka kwenye ndege hiyo.

Wanafunzi hao manusura wa ajali iliyotokea mwezi wa tano wamelakiwa na umati wa watu wakiwamo Wanafunzi wenzao wa  shule ya Lucky Vicent.

.