Mfumo wa uondoaji shehena bandarini pasua kichwa

Muktasari:

  • Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa wakuu wa taasisi za Serikali wanaohusika na udhibiti wa mizigo katika maeneo hayo na wadau mbalimbali wa sekta binafsi, kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alisema lengo la kuwashirikisha ni kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji.

Dar es Salaam. Serikali imeanza maandalizi ya kutengeneza mfumo wa pamoja wa kielektroniki wa uondoaji shehena bandarini, viwanja vya ndege na mipakani kwa lengo la kuboresha utendaji na ufanisi.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa wakuu wa taasisi za Serikali wanaohusika na udhibiti wa mizigo katika maeneo hayo na wadau mbalimbali wa sekta binafsi, kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alisema lengo la kuwashirikisha ni kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji.

Naye mratibu wa mfumo huo wa TRA, Felix Tinka alizitaja faida zitakazopatikna kuwa ni kurahisisha na kuwezesha biashara, kuongeza ufanisi wa matumizi bora ya rasilimali na kuongeza uhiari wa ulipaji ushuru na tozo mbalimbali.

kwa waingizaji na waondoshaji wa mizigo.