Magufuli akabidhi kombe la ubingwa Simba VPL 2017/18

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli ameitaka Simba iimarishe kiwango chake cha uchezaji ili ifanye vizuri kwenye mashindano ya Kimataifa.

Akizungumza katiba hotuba yake fupi kabla ya kuikabidhi timu hiyo Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu baada ya kumaliza mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar, Rais Magufuli alisema kiwango cha Simba katika mchezo wa jana kinatoa ishara mbaya kuelekea mashindano ya kimataifa.

"Mimi nataka kuona timu za Tanzania zinafanya vizuri pale zinaposhiriki mashindano ya Afrika. Niseme ukweli kwamba kama Simba itacheza kwa kiwango hiki cha leo basi haiwezi kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa.

Kwa hiyo mkae chini na muhakikishe mnajiandaa vizuri ili kuongeza kiwango chenu vinginevyo hamuwezi kufanya vizuri," alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia amehimiza ujenzi na utunzaji wa miundombinu ya michezo katika miji ili kuunga mkono juhudi za kuendeleza sekta hiyo.

"Nazishauri halmashauri zote  nchini kuhakikisha kutenga maeneo ya   michezo na kuhakikisha hayavamiwi. Ni imani yangu kwamba sekta ya michezo itaendelea kukua," alisema Rais Magufuli.

Rais pia alikitaka Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha kinatunza viwanja vyake ambavyo haviko katika hali nzuri.

"Tunawaomba ndugu zetu wa CCM ambao wanamiliki viwanja vingi wahakikishe wanavitunza.

"Sambamba na hilo tutaendelea kujenga miundombinu ya michezo. Kama mnavyofahamu hivi karibuni tutajenga uwanja wa kimataifa wa michezo kuel Dodoma kwa kushirikiana na wenzetu wa Morocco.