Fifa kutoa mgawo wa Sh13 bilioni Kwa kila nchi

Muktasari:

Kila mwaka shirikisho hilo hutoa ruzuku kwa wanachama wake kwa ajili ya kujsaidia programu za vijana; mafunzo ya walimu, waamuzi, madaktari, viongozi; vifaa na mashindano ya vijana na wanawake.

 


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino ameauambia mkutano mkuu unaoendelea jijini Moscow, Urusi kuwa kila nchi mwanachama itapata dola 6 milioni za Kimarekani (sawa na zaidi ya Sh13 bilioni) kwa ajili ya kusaidia programu za maendeleo ya mchezo huo.

Rais huyo alitoa ahadi hiyo katika hotuba yake ya ufunguzi kwenye mkutano huo unaofanyika siku moja kabla ya fainali za Kombe la Dunia kuanza.

Jnfantino amesema nchi zote wanachama 211 wa FIFA zitanufaika na mgawo huo katika kusaidia programu mbalimbali za kukuza mchezo wa mpira wa miguu.