ACT, Chadema wajitosa ugomvi wa CUF

Muktasari:

Ugomvi huo ni kati ya mshauri wa ACT, Profesa Kitila Mkumbo na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ambao jana walitupiana maneno na kejeli za kisiasa kuhusu mgogoro huo unaohusisha mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na upande mwingine unaoongozwa na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

Dar es Salaam. Wakati mnyukano wa kisiasa ukiendelea ndani ya CUF, makada wa vyama vya ACT – Wazalendo na Chadema wamenunua ugomvi huo na kurushiana lawama mtandaoni.

Ugomvi huo ni kati ya mshauri wa ACT, Profesa Kitila Mkumbo na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ambao jana walitupiana maneno na kejeli za kisiasa kuhusu mgogoro huo unaohusisha mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na upande mwingine unaoongozwa na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

Kilichomwibua Lissu ni kauli ya Profesa Mkumbo kwamba CUF ya Profesa Lipumba na nje ya Ukawa itakuwa chama imara. Lakini Lissu alimjibu Profesa Kitila kuwa anajua kuwa hoja yake hiyo ni uchwara isiyokuwa na msingi wowote katika hali halisi.