ATE:Bado kuna unyanyapaa wa wenye VVU makazini

Muktasari:

Kutokana na changamoto hiyo Chama cha Waajiri (Ate) kimewataka waajiri katika maeneo mbalimbali ya kazi kuhakikisha inakabiliana na hali hiyo ili kutoa nafasi kwa wafanyakazi waathirika kuonyesha mchango wao.

Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa bado kuna unyanyapaa kwa waathirika wa Ukimwi katika sehemu za kazi. 

Kutokana na changamoto hiyo Chama cha Waajiri (Ate) kimewataka waajiri katika maeneo mbalimbali ya kazi kuhakikisha inakabiliana na hali hiyo ili kutoa nafasi kwa wafanyakazi waathirika kuonyesha mchango wao. 

Agizo hilo limetolewa leo wakati  katika mkutano uliowakutanisha maofisa rasilimali watu kutoka katika taasisi mbalimbali nchini.