Mtulia kupambana na aliyekuwa meneja wake

Mgombea ubunge wa Cuf Jimbo la Kinondoni, Rajabu Salim Juma akitambulishwa na Abdul Kambaya. Picha na Salim Shao

Muktasari:

Alimsaidia kushinda akiwa CUF sasa kupambana naye akiwa CCM

Dar es Salaam. Aliyekuwa meneja kampeni wa Maulid Mtulia kwenye uchaguzi wa 2015 Kinondoni, Rajabu Salim Jumaa leo Alhamisi amechukua fomu kugombea ubunge jimbo hilo.

Mwaka 2015 mgombea wa CUF Mtulia alishinda ubunge wa jimbo hilo lakini alijivua uanachama wa CUF na kuhamia CCM na hivyo kupoteza sifa ya ubunge.

Akizungumza leo Alhamisi, Juma amesema atamshinda Mtulia katika nafasi hiyo kwa sababu anaisababishia Serikali hasara.

"Gharama kubwa za uchaguzi zinasababishwa na Mtulia ambaye alishakuwa mbunge lakini amejiuzulu na kutaka tena ubunge.”