Balozi Kijazi aitaka ATCL ijipange

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi

Muktasari:

Kijazi amehutubia katika uzinduzi wa ndege mbili za Bombadier Q 400 unaofanyika Uwanja wa Julius Nyerere  ambako Rais John Magufuli atazizindua hivi punde.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, amesema  ndege mbili mpya zilizonunuliwa na serikali si za ATCL bali ni za serikali na shirika hilo litaingia mkataba kwa kukodishwa na kulitaka lijipange vyema kibiashara.

Kijazi amehutubia katika uzinduzi wa ndege mbili za Bombadier Q 400 unaofanyika Uwanja wa Julius Nyerere  ambako Rais John Magufuli atazizindua hivi punde.

Wakati huo huo Spika wa bunge, Job Ndugai amemshukuru Rais wa kuwatoa kimasomaso watanzania

“Tulikuwa na aibu kubwa, tulikuwa tunagombana bungeni ni matumaini yetu Twiga hawa watatunzwa na hawatatumia njia za kizamani, sisi bungeni tumejipanga tuna kamati tatu za kuwasimamia,” alisema Ndugai.

Nuzulack Dausen, anaendelea kuripoti taarifa hii akiwa JNIA.