Ben Pol na Ebitoke waendeleza sinema za mahaba

Muktasari:

Hivi karibuni,zilienea taarifa kuwa Ebitoke anamtaka kimapenzi Ben Pol.

Juzi, Benpol alionyesha  kulikubali ombi la mchekeshaji Ebitoke na sasa  Ebitoke ameanza kummwagia sifa Ben Pol.

Msanii wa Bongo Flavor, Ben Pol na mchekeshaji anayeibukia kwa kasi, Ebitoke, wameendeleza sinema zao katika mitandao ya kijamii.

Hivi karibuni,zilienea taarifa kuwa Ebitoke anamtaka kimapenzi Ben Pol.

Juzi, Benpol alionyesha  kulikubali ombi la mchekeshaji Ebitoke na sasa  Ebitoke ameanza kummwagia sifa Ben Pol.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ebitoke ameendelea kuonyesha wazi hisia alizonazo juu ya Ben Pol huku akimmwagia sifa mbalimbali juu ya mambo anayoendelea kufanyiwa.

Mapema juzi Ebitoke aliposti video iliyomuonyesha akiwa katika sherehe akipiga picha na watu mbalimbali huku nyuma yake kukiwa na wanaume wawili walioonekana kama walinzi wakimfuata kila aendako na baadaye aliweka picha nyingine iliyoambatana na maneno yaliyosomeka.

“Umeahidi kunihakikishia ulinzi 24 hours na umetimiza, thank you my king” aliandika Ebitoke.