Benki ya KCB kuwezeshwa wanawake 315

Muktasari:

Programu hiyo inayotekelezwa kwa ushirikiano na Kituo cha Ujasiriamali Tanzania (TECC), itaendeshwa kwa miezi sita na kutoa mafunzo, ushauri na mikopo ya kuendeleza biashara za washiriki

Dar es Salaam. Benki ya KCB kupitia programu yake ya Tujiajiri imepanga kuwajengea uwezo wa kijasiriamali wanawake 315 kuchangamkia fursa na kuondokana na umaskini.

Programu hiyo inayotekelezwa kwa ushirikiano na Kituo cha Ujasiriamali Tanzania (TECC), itaendeshwa kwa miezi sita na kutoa mafunzo, ushauri na mikopo ya kuendeleza biashara za washiriki.

Akiielezea programu hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa alisema: “KCB inakusudia kuwawezesha wanawake kukabiliana na changamoto zinazowakabili ili kukuza biashara zao kwa uchumi wa taifa.”