Polisi wadaka bidhaa zilizoisha muda bandari kavu

Muktasari:

Bidhaa hizo ni pamoja na sukari na mafuta ya kula na zilikuwa zikisafirishwa kwa kutumia majahazi

 Polisi wamekamata bidhaa ambazo zimeisha muda wake wa matumizi zikiingizwa nchini kupitia bandari bubu ya Kigombe.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe amesema kuwa bidhaa hizo zikiwamo kanga, sukari, mafuta ya kula na bidhaa nyingine zimekuwa zikiingizwa kutoka nchi za nje zikipitia Bandari ya Zanzibar.

Amesema bidhaa hizo ni mifuko 307 ya sukari ya uzani wa kilo 50 kila mmoja, madumu 270 ya mafuta ya kula kila moja likiwa na lita 20, vitenge pamoja na kanga.

Amesema  askari wa jeshi hilo waliokuwa  katika doria kwenye Bahari ya Hindi wamekutana na majahazi matatu yanayosadikika kubeba mali za magendo ambapo mawili kati yao yalinaswa.

 

“Kazi ya kuwakamata baharini ilikuwa ngumu askari walilazimika kutumia mabomu ya machozi, lakini hata hivyo miongoni mwao walifanikiwa kutoroka,” amesema Bukombe.

 

Amesema kuwa sukari hiyo imeingizwa nchini kutoka Msumbiji na Brazil wakati mafuta hayo yametokea nchini Indonesia na baada ya kukamatwa baharini yalishushiwa bandari bubu ya Kigombe wilayani

Muheza.