Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Binti darasa la tatu adaiwa kubakwa akienda shule

Muktasari:

Mtuhumiwa akamatwa, adai alikuwa akimpa vifaa vya shule


Muleba. Mwanafunzi wa darasa la tatu wa Shule ya Msingi Kagoma wilayani Muleba mkoani Kagera (jina tunahifadhi) anadaiwa kubakwa leo asubuhi wakati akielekea shuleni.

Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Kagoma, Patrick Luhosho amesema mtuhumiwa amekamatwa na anahojiwa akihusishwa na tukio hilo.

Luhosho amesema inasemekana mtuhumiwa alimuita mwanafunzi na kuingia naye ndani ya nyumba ambapo watu waliofuatilia walizingira nyumba na kumkuta amemshikilia mwanafunzi ambapo walimkamata kumfikisha ofisi ya kijiji.

"Niliona wanataka kumdhuru nikaita polisi kuomba msaada wa kiusalama, niliyempigia alikuwa njiani akienda Muleba mjini ndipo wakamchukua kwa ajili ya kuhojiwa," amesema Luhosho.

Mzazi wa mwanafunzi huyo (jina linahifadhiwa) amesema kwa sasa yuko katika zahanati akisubiri binti yake afanyiwe uchunguzi.

 

"Muda huu niko Zahanati ya Izigo na askari polisi nasubiria majibu ya mganga, kitakachobainika nitakupigia kukwambia nilichoelezwa ikiwemo hali ya mtoto kiafya," amesema.

 

Baadhi ya mashuhuda wamesema mtuhumiwa ni mfanyabiashara wa bidhaa ndogondogo za duka na inadaiwa alipohojiwa na wananchi alidai alikuwa akimpatia mwanafunzi huyo vifaa vya shule.