BoT yaiangukia NHC

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu .

Muktasari:

  • Profesa Ndulu alitoa ombi hilo jana, wakati akikabidhiwa nyumba 10 za watumishi wa benki hiyo kutoka NHC. “Mimi niwaombe NHC kuhakikisha ifikapo mwishoni mwa Septemba, tukabidhiwe nyumba zote ili watumishi ambao watahamia wafikie kwenye nyumba hizo,” alisema.

Mtwara. Hakuna kitu kinachokamilika bila kutegemea kingine, hiyo inaweza kujidhihirisha baada ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu kuliomba Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kukamilisha ujenzi wa nyumba 40 zilizobaki eneo la Raha Leo Manispaa ya Mikindani Mtwara ifikapo Septemba.

Profesa Ndulu alitoa ombi hilo jana, wakati akikabidhiwa nyumba 10 za watumishi wa benki hiyo kutoka NHC. “Mimi niwaombe NHC kuhakikisha ifikapo mwishoni mwa Septemba, tukabidhiwe nyumba zote ili watumishi ambao watahamia wafikie kwenye nyumba hizo,” alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu alisema kutokana na  Mtwara kuwa na fursa lukuki za uchumi,  shirika hilo limejenga nyumba za makazi 125 eneo la Raha Leo Manispaa ya Mikindani Mtwara. 

Hata hivyo, Mchechu alisema  mradi wa ujenzi wa nyumba hizo utakapokamilika watakuwa wametumia Sh30 bilioni.