Bodaboda wapewa mwezi kuacha kudeka

Waendesha pikipiki (bodaboda wakiwa kwenye majukumu yao

Muktasari:

Agizo hilo lilitolewa jana kwenye kikao kilichowakutanisha waendasha pikipiki za abiria, uongozi wa halmashauri, Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani na Sumatra.

Pwani. Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) Mkoa wa Pwani, kwa kushirikiana  na Halmashauri ya Mji Kibaha, imewapa mwezi mmoja kuanzia juzi wamiliki wa pikipiki na bajaji kukata leseni ya usafirishaji abiria.

Agizo hilo lilitolewa jana kwenye kikao kilichowakutanisha waendasha pikipiki za abiria, uongozi wa halmashauri, Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani na Sumatra.

Ofisa Leseni wa Sumatra Mkoa wa Pwani, Mwasi Christian alisema kinachofanyika ni utekelezaji wa sheria inayoeleza umuhimu wa leseni ya usafirishaji abiria.

Hata hivyo, waendesha  bodaboda  walisema muda wa mwezi mmoja waliopewa ni mfupi na kuomba kuongezewa miezi mitatu, ombi hilo lilipingwa na Sumatra.