Buhari kurudi Nigeria

Muktasari:

Kutokuwepo kwake nchini Nigeria kulisababisha wasiwasi mkubwa katika taifa hilo lionaloongoza kiuchumi barani Afrika

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anatarajiwa kurudi nchini kwake leo akitokea London Uingereza  alipokuwepo kwa siku 100 akipatiwa matibabu.

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, atarejea leo baada ya kumaliza  matibabu mjini London Uingereza.

Taarifa zilizotolewa na Ikulu ya Uingereza leo zimesema kwamba ,Buhari mwenye umri wa miaka 74 alikuwa akipata matibabu  Uingereza kwa zaidi ya siku 100.

Hata hivyo taarifa hiyo haikusema kwamba kiongozi huyo anasumbuliwa na ugonjwa gani.