CCM waijibu Chadema operesheni Ukuta

Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka. Picha ya mtandao

Muktasari:

  • Taarifa iliyotolewa jana na msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alisema kuwa kutokana na kasi ya Rais John Magufuli wapinzani wamekosa ajenda hivyo njia pekee wanayoona ili waendelee ili kufanya utapeli ni kutunga uongo.
  • Jana Chadema kupitia Mbowe walitangaza kuwa Septemba Mosi mwaka huu kupitia operesheni yao iitwayo Ukuta.

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi(CCM) kimeijibu Chadema kwa kueleza kuwa tamko la Chadema lililotolewa jana na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe limejaa uongo mwingi na ghiliba za kibabaishaji.

Taarifa iliyotolewa jana na msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alisema kuwa kutokana na kasi ya Rais John Magufuli wapinzani wamekosa ajenda hivyo njia pekee wanayoona ili waendelee ili kufanya utapeli ni kutunga uongo.

Jana Chadema kupitia Mbowe walitangaza kuwa Septemba Mosi mwaka huu kupitia operesheni yao iitwayo Ukuta.