CCM yavunja ukimya mauaji Pwani

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole

Muktasari:

  • Hadi sasa zaidi ya watu 30 wamepoteza maisha kutokana na mauaji hayo.

Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekemea vikali mauaji yanayotokea mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo, Alhamisi   Polepole amesema kuwa kama CCM wanataka kuona mauaji hayo yanaendelea kukemewa zaidi.

Polepole ameonyesha  masikitiko yake kwa vyama vya upinzani kukaa kimya badala ya kuungana kama Taifa kukemea mauaji ya watendaji wa CCM yanayoendelea mkoani Pwani.

"Kuungana kwenye ruzuku, hapana vyama vinapaswa kuwa na umoja katika masuala mbalimbali ikiwamo mauaji hayo," amesema Polepole.