CDA yapima viwanja vya makazi, uwekezaji

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi

Muktasari:

Akizungumza jana, Mkurugenzi Mkuu wa CDA, Paskas Mulagiri alisema wananchi watakaohitajika kulipwa fidia watalipwa.

Dodoma. Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) imekamilisha mpango wa kupima viwanja 20,000 kwa ajili ya ujenzi wa makazi na vitega uchumi.

Akizungumza jana, Mkurugenzi Mkuu wa CDA, Paskas Mulagiri alisema wananchi watakaohitajika kulipwa fidia watalipwa.

“Tunakamilisha mpango wa maandalizi ya ndani kwa ajili ya upimaji huo utakaozalisha viwanja vya kawaida 20,000,” alisema.

Hata hivyo, alikataa kutajamaeneo viliko viwanja hivyo ili kuondoa usumbufu wa watu kwenda kuvamia kushinikiza kulipwa fidia.

Alisema baada ya kukamilisha kupima viwanja hivyo, mamlaka hiyo itatoa taarifa na kutangaza bei kulingana na ukubwa.

Kuhusu viwanja vya uwekezaji, Mulagiri alisema viko maeneo ya Njadengwa na Kizota WIA Extension ambako wamepokea maombi mengi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi (apartment) na viwanda.