Chadema Temeke wamfukuza uanachama diwani wa Kurasini

Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo( Chadema) wilaya ya Temeke kimemfukuza uanachama Diwani wa Kata ya Kurasini ambaye ni  mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa  Mivinjeni , Matiti Togocho kwa kile walichodai kuwa amekuwa akifanya ufisadi ikiwemo kutengeneza hati za viwanja feki na kujipatia kipato.
Mwenyekiti Chadema wilaya hiyo Berdad Mwakyembe amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na makosa ya ufisadi aliyowafanyia wananchi wa kata yake.
Mwakyembe alisema diwani huyo ameshindwa kuwaletea maendeleo wananchi wake badala yake alikuwa anatumia nafasi yake kujinufaisha huku akiwawakandamiza wananchi wanyonge.
Hata hivyo Diwani Togocho alisema hatozungumzia suala hiko hadi atakapopewa ruhusa kutoka kwa mratibu wa kanda kuongea suala hilo
“Unajua aliyeongea mwenyekiti wangu hivyo siwezi kuropoka kitu hadi nisikilize mabosi wangu ambaye mratibu wa kanda,”alisema Togocho