Chadema watangaza mikutano ya hadhara kuanzia Septemba Mosi

Muktasari:

Chama hicho pia kimezindua Operesheni Ukuta (Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania),  huku kikiwataka wananchi wote waliokumbana na 'rungu'  la Serikali ya Awamu ya Tano kuungana na Operesheni hiyo,  wakiwemo mama ntilie na waendesha bodaboda.

Dar es Salaam. Kufuatia kile walichokiita 'matukio ya ukandamizaji wa haki na demokrasia',   Chadema kimetangaza Septemba Mosi mwaka huu kuwa siku ya mikutano ya hadhara nchi nzima.

Chama hicho pia kimezindua Operesheni Ukuta (Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania),  huku kikiwataka wananchi wote waliokumbana na 'rungu'  la Serikali ya Awamu ya Tano kuungana na Operesheni hiyo,  wakiwemo mama ntilie na waendesha bodaboda.

Chama hicho kimetaja mambo 11 kinachodai kuwa yamefanywa na Serikali bila kufuata sheria na kanuni za nchi,  likiwemo la kuzuiwa kwa shughuli za kisiasa na kutaja sababu 24 za kuibuka na Operesheni Ukuta