Chadema yazindua sera mpya

Mwenyekiti wa chadema Freeman Mboe na katibu mkuu wa chama hicho Vicent Mashinji wakikata utepe kuzindua sera za Chama hicho wengine kulia ni Naibu katibu mkuu zanziba Salum Mwalim na Kushoto ni Naibu katibu Mkuu Bara John Mnyika. Picha na Said Khamis

Muktasari:

  • Kabla ya kutayarisha sera mpya iliyozinduliwa leo Septemba 25,2018 ambayo imegawanyika kwenye maeneo makuu matatu na kufafanuliwa kwenye maeneo  12, Chadema walitumia mwaka mzima kufanya tafiti, kukusanya mawazo kutoka kwa watu mbalimbali wakiwamo wataalamu lengo likiwa ni kupata kitu kizuri kitakachosaidia kusogeza jamii ya Watanzania kutoka eneo moja kwenda lingine.


Dar es salaam. Chadema imezidua sera mpya ya mwaka 2018 iliyogawanyika kwenye maeneo matatu.

Akizungumza leo Septemba 25, 2018 wakati wa uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema sera hizo zitakuwa zinafanyiwa marekebisho kulingana na wakati.

Amesema eneo la kwanza lililoko kwenye sera hiyo ni ile inayolinda uhuru wa wananchi.

Mbowe amesema Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kuzungumzia suala la maendeleo ya watu na uhuru, jambo ambalo wamelijadili kwa kina kwenye sera hiyo.

Amelitaja eneo lingine ni nafasi kuwa na sera zinazolenga misingi ya uchumi.

Amesema katika eneo hilo wameainisha ni kwa namna gani wananchi watapata huduma za kijamii.

Amefafanua eneo hilo limeainisha namna uchumi utakavyokuwa endelevu badala ya kuwa uliohodhiwa na Serikali.

Mbowe ameitaja sera nyingine ni zinazoilinda na kuihuisha jamii kupata huduma ya maji, barabara yasiwe mambo yanayofanywa na sekta binafsi bali yafanywe na Serikali.

"Sasa hivi kumejengeka dhana kuwa Serikali uliyojenga shule, zahanati inakuwa ni kama msaada, hii si sawa hayo ni majukumu ya Serikali," amesema Mbowe.

Mbowe amesema kabla ya kutayarisha sera hiyo wametumia mwaka mzima kufanya tafiti na kukusanya maoni kutoka kwa watu mbalimbali.