VIDEO: Chidi Benzi adaiwa kukutwa na gramu tano za Bangi

Msani wa Muziki wa Kizazi Kipya, Chid Benzi (katikati) akiwa chini ya ulinzi katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dodoma leo akituhumiwa kukamatwa na dawa za kulevya aina ya bangi. Na Mpigapicha Wetu

Muktasari:

Kamanda Muroto amesema kuwa Chidi benz atafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.


Dodoma. Polisi mkoani Dodoma inamshikilia mwanamuziki wa Hip Hop Chidi Benzi kwa tuhuma za kukutwa na bangi gramu tano.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 18,   Kamanda wa polisi Dodoma Gilles Muroto amesema Chidi Benz amekamatwa mwishoni mwa wiki katika eneo la mji Mpya Jijini Dodoma.

Kamanda Muroto amesema kuwa Chidi benz atafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.

Miongoni mwa nyimbo zilizompa umaarufu Chid Benz ni pamoja na Ngoma Itambae, Mmenisoma, Naitwa Nani, Hasira za Nini na Mashallah.