DC awatupia lawama wanasiasa

Muktasari:

Alisema wanasiasa ndiyo waliosababisha vijiji 36 vilivyo ndani ya hifadhi kusajiliwa, ingawa hadi sasa kati ya hivyo, 11 tayari vimefutiwa usajili

Kaliua. Mkuu wa Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, Abel Busalama amewatupia  lawama wanasiasa kwa kushawishi wananchi kuvamia hifadhi za misitu, huku akiagiza kuwatenga kwa kutopelekewa huduma za jamii.

Busalama alisema tayari maeneo mengi, wavamizi wameamriwa kuondoka kwa hiari na wamenza kutekeleza  agizo hilo na kwamba, wanaokaidi wataondolewa kwa nguvu.

Alisema wanasiasa ndiyo waliosababisha vijiji 36 vilivyo ndani ya hifadhi kusajiliwa, ingawa hadi sasa kati ya hivyo, 11 tayari vimefutiwa usajili.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, John Pima alisema maeneo ya kuishi yapo na wanaruhusiwa kuhamia, kinachotakiwa ni kufuata masharti ya sehemu na vijiji wanavyotaka.