Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dawa za maumivu zaumiza wengi

Muktasari:

Utafiti huo umebaini kwamba dawa za kupunguza maumivu kama Brufen zinaongeza uwezekano wa kusababisha kifo kwa zaidi ya asilimia 20, kutokana na shambulio la moyo ‘heart attack’.

Dar es Salaam. Dawa za maumivu zimetajwa kuwa chanzo cha ongezeko la vifo vya ghafla vitokanavyo na shambulio la moyo, utafiti uliochapishwa na jarida la kitabibu la Scientist Daily la Uingereza limebainisha.

Utafiti huo umebaini kwamba dawa za kupunguza maumivu kama Brufen zinaongeza uwezekano wa kusababisha kifo kwa zaidi ya asilimia 20, kutokana na shambulio la moyo ‘heart attack’.

Utafiti huo unashauri kuwa ni vyema wagonjwa ambao wanaandikiwa dawa za kutuliza maumivu, wakatumia kiwango kidogo cha dozi na kujitahidi kutozitumia mara kwa mara.

Pia, utafiti huo umeonya wanaopenda kununua dawa hizo wakati wowote kwenye maduka bila kufuata ushauri wa daktari.