Diwani aahidi kuacha kazi wananchi wasipopata maji

Muktasari:

  • Esther ameiomba  halmashauri na mkoa  kwa ujumla kuwaona kwa jicho la huruma wanakijiji hicho ili waonje matunda ya uhuru.

Mbeya. Diwani wa Kata ya Mshewe, Halmashauri ya Mbeya Vijijini,  Esther Mbega amesema ataacha udiwani kama Serikali haitapeleka maji  katika Kijiji cha Ilota ambacho  wananchi wanaamka saa 9.00 usiku kwenda kutafuta maji umbali wa kilometa 10.

Esther ameiomba  halmashauri na mkoa  kwa ujumla kuwaona kwa jicho la huruma wanakijiji hicho ili waonje matunda ya uhuru.

Akizungumza na mwandishi, diwani huyo alisema  changamoto hiyo ni kubwa na ya siku nyingi huku akisisitiza kwamba ataacha wadhifa huo kama  Serikali haitafikisha huduma ya maji safi na salama katika kijiji hicho.

"Sitaona sababu ya kuendelea na nafasi hii kama Serikali haitaona umuhimu wa kuleta maji katika kijiji hiki kwani wananchi wangu wanatabika ,ndoa zinavunjika, wajawazito wanataabika kusaka maji, "alisema.

Kwa habari zaidi nunua gazeti la Mwananchi kesho, kwa walio mbali wanaweza kujiunga na  epaper yetu kwa kubonyeza hapa