Diwani wa Chadema Moshi atiwa hatiani kwa kumshambulia polisi

Muktasari:

  • Mbali na kumtia hatiani kwa kosa hilo, lakini mahakama hiyo chini ya Hakimu Mkazi, Idan Mwilapo pia ilimtia hatiani diwani huyo na washirika wake wengine watatu kwa kosa lingine la kumzuia polisi huyo kufanya kazi yake.

Moshi. Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Kilimanjaro, imemtia hatiani Diwani wa kata ya Pasua mjini Moshi kwa tiketi ya Chadema, Charles Mkalakala (47) kwa makosa mawili likiwamo la kumshambulia Polisi.

Mbali na kumtia hatiani kwa kosa hilo, lakini mahakama hiyo chini ya Hakimu Mkazi, Idan Mwilapo pia ilimtia hatiani diwani huyo na washirika wake wengine watatu kwa kosa lingine la kumzuia polisi huyo kufanya kazi yake.

Hukumu hiyo imetolewa leo ambapo kwa kosa la kumshambulia Polisi huyo, Diwani huyo alihukumiwa kulipa faini ya Sh 500,00 na kumlipa polisi huyo fidia ya Sh 400,000 au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.

Katika kosa la pili lililomhusisha Diwani huyo na washitakiwa, Hussein Mkalakala (21), Fikra Said (23) na Raymond Andrea(34), Mahakama iliwahukumu kulipa faini ya Sh400,000 kila mmoja.