Diwani wa chadema afikishwa mahakamani

Muktasari:

Akisomewa shauri hilo mbele ya Hakimu Mfawidhi Augustino Rwezire, mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Arusha, diwani huyo anakabiliwa na shitaka la kuhamasisha wananchi kufanya maandamanao yasiyo halali, Septemba mosi

Arusha. Diwani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kata ya Sombetini,Ally Bananga(40),amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuhamasisha uchochezi

Akisomewa shauri hilo mbele ya Hakimu Mfawidhi Augustino Rwezire, mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Arusha, diwani huyo anakabiliwa na shitaka la kuhamasisha wananchi kufanya maandamanao yasiyo halali, Septemba mosi  

Diwani huyo amefikishwa mahakamani hapo leo mbele ya Hakimu Mfawidhi,Agustino Rwizile,ambapo Wakili wa Serikali Charles Kagirwa,alidai kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Agosti 13 mwaka huu,wilayani Karatu mkoa wa Arusha.

Pia amesema  kuwa siku ya tukio Bananga akiwahutubia wananchi katika mkutano wa wazi uliofanyika eneo la Hosteli ya Karatu, aliwahamasisha wananchi hao washiriki katika kusanyiko lisilo halali Septemba Mosi.

Wakili huyo ameiomba mahakama  kuahirisha kesi hiyo kutokana na upelelezi wake kutokukamilika na kudai kuwa dhamana iko wazi kwa mshitakiwa.

Mawakili wa utetezi  John Mallya Wakili James Lyatuu, wameiomba mahakama hiyo kumpa Bananga  masharti nafuu ya dhamana kwani ni diwani na anaweza kujidhamini mwenyewe
Hakimu Rwizile alikubaliana na ombi hilo  na kumtaka Diwani huyo kujidhamini mwenyewe kwa dhamana ya shilingi 5 milioni na kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 22 mwaka huu ambapo kesi hiyo itatajwa tena.
Diwani huyo alitiwa kizuizini kwa siku tatu huku nyumbani kwakwe kukutwa na fulana moja iliyoandikwa UKUTA