Thursday, June 14, 2018

Dk Mpango: Rais alinitwisha msalaba wa zege

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akiwasilisha bungeni Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi 

By Kalunde Jamal, Mwananchi kjamal@mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango, Phillip Mpango ameanza kusoma bajeti  kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19, huku akieleza kuwa licha ya kuitwa mbahili lakini Rais John Magufuli alimtia moyo.

Akiwasilisha bajeti hiyo leo Juni 14 bungeni, Dk Mpango amesema Rais Magufuli alimtwisha msalaba wa zege lakini ameubeba ili kuokoa walio wengi hasa wanyonge.

“Ilikuwa ni lazima wachache kuumia ili wengi waokolewe,” amesema.

Ametaja mengi aliyofanya Rais Magufuli  kwa mwaka wa fedha 2017/18 kuwa ni pamoja ununuzi wa ndege sita na ujenzi wa reli ya kisasa ya Stieglers Gauge.

“Baadaye zitawasili ndege nyingine mbili kubwa aina ya Boeing, Dreamliner,” amesema

Endelea kufuatilia habari Zaidi zinakujia

 

 


-->