Dk Tizeba: Nimetumwa na JPM kudhibiti uvuvi haramu

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba

Muktasari:

Hivyo, watu wote wanaojihusisha na shughuli hiyo ameagiza wakamatwe au kusalimisha zana zao.

Buchosa. Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba amesema Rais John Magufuli alimpatia wizara hiyo kwa lengo la kupambana na kudhibiti watu wanaojihusisha na uvuvi haramu ndani ya Ziwa Victoria na maziwa mengine nchini.

Hivyo, watu wote wanaojihusisha na shughuli hiyo ameagiza wakamatwe au kusalimisha zana zao.

Waziri huyo ametoa siku 30 kwa maofisa uvuvi kuwasilisha majina ofisini kwake ya watu wanaojihusisha na uvuvi haramu katika Ziwa Victoria.

Alitoa agizo hilo juzi alipofanya ziara wilayani Sengerema mkoani Mwanza. Dk Tizeba alisema watakaokaidi kuwasilisha majina hayo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

 “Kuna malalamiko kutoka kwa maofisa uvuvi kuwatupia lawama wananchi kuwa wanawakumbatia watu wanaojihusisha na uvuvi haramu katika maeneo yao kutokana na kuingia naomkataba wa kila mwezi kwa kuwalipa Sh100,000, lazima wahusika hao wakamatwe,” alisema Dk Tizeba.