Fursa zitumike kutoa ajira

Muktasari:

Katibu wa Ofisi ya Mbunge wa Ilemela, Kheri James akizungumza na wajasiriamali kwenye Kata ya Nyamanoro amesema inashangaza wananchi wa eneo hilo kushindwa kutumia fursa zinazopatikana.

Mwanza. Vijana wameshindwa kuzitumia fursa zilizopo kujiajiri na kuondokana na hali ngumu ya maisha hivyo kukosa kipato.

Katibu wa Ofisi ya Mbunge wa Ilemela, Kheri James akizungumza na wajasiriamali kwenye Kata ya Nyamanoro amesema inashangaza wananchi wa eneo hilo kushindwa kutumia fursa zinazopatikana.

“Kuna ziwa, soko la samaki la kimataifa la Mwaloni Kirumba, uwanja wa ndege, jengo la Rock City Mall, Uwanja wa CCM Kirumba na viwanda, hizi ni baadhi ya fursa zinazotuzunguka,” amesema.