Gharama Mwendokasi zapunguza wafanyakazi

Muktasari:

Nauli za mabasi hayo yaliyolenga kupunguza foleni jijini Dar es Salaam, zilitangazwa Mei 9, ikiwa ni siku moja kabla ya uzinduzi wa safari zake.

Dar es Salaam. Wakati Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi Dar es Salaam (Dart) ukiwa umefikisha siku 158 tangu ulipozinduliwa Mei 10, kampuni inayouendesha imelazimika kupunguza wafanyakazi kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa.

Nauli za mabasi hayo yaliyolenga kupunguza foleni jijini Dar es Salaam, zilitangazwa Mei 9, ikiwa ni siku moja kabla ya uzinduzi wa safari zake.

Nauli hizo zilizotangazwa na mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Majini na Nchi Kavu (Sumatra), Johansen Kahatano ni Sh800 kutoka Mbezi Mwisho hadi Kivukoni na wanafunzi ni Sh200.

Nauli kutoka Mbezi Mwisho-Kimara hadi Kariakoo Sh800 na Kutoka Morocco - Kimara hadi Mbezi Mwisho ni Sh800 na kutoka Morocco - Kivukoni Sh650, sawa na Kariakoo hadi Morocco.

Lakini nauli hizo zinazonekana kutokidhi gharama za uendeshaji.  Katika kutathmini siku 158 tangu kuanza kwa huduma hiyo, Mwananchi ilizungumza na David Mgwassa, mkurugenzi mtendaji wa Udart inayoendesha mradi huo ambaye alisema gharama za uendeshaji ni kubwa kuliko mapato.

“Kwa siku tunapakia abiria 120,000, lakini gharama za uendeshaji ni kubwa kuliko mapato kwa sababu nauli tuliyopewa ni chini ya ile tuliyoomba na iliyowekwa kwenye mkataba,” alisema Mgwasa.

Habari zaidi soma Gazeti la Mwananchi