HESLB yapewa mbinu za kuwasaka wakopaji

Dar es Salaam. Jumuia ya Taasisi za Mikopo ya Elimu ya Juu Afrika (AAHEFA) imeishauri Bodi ya Mikopo Tanzania (HESLB) kutumia mfumo wa smartcard ili kukabiliana na changamoto ya ukusanyaji wa mikopo inayotolewa kwa wanafunzi.

Rais wa Jumuia hiyo, Charles Ringera alisema katuka mfumo huo hutolewa kadi ambayo huunganishwa mawasiliano ya mkopaji na hati yake ya kusafiria ili kuiwezesha HESLB kujua taarifa sahihi za mhitimu pindi itakapohitaji kurejeshewa mkopo.