Hakuna jipya Mpango wa Maendeleo -Silinde

Mbunge wa Momba (Chadema) David Silinde

Muktasari:

  • Akitoa maoni jana kuhusu Mpango wa Maendeleo wa Taifa, Kiwango na Ukomo wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2017/18, Silinde alisema katika miezi tisa, Serikali imetekeleza asilimia 26 kwa kupeleka fedha za miradi ya maendeleo.
  • “Hawawezi kumaliza asilimia 74 zilizobaki katika kipindi cha robo mwaka kilichobaki,” alisema.
  • Alisema hali hiyo inatokana na sababu nyingi, ikiwamo makusanyo ya ndani ya nchi kutumika kulipa mishahara na madeni

Dodoma. Mbunge wa Momba (Chadema) David Silinde amesema haoni jambo jipya katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa sababu utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17 katika miradi ya maendeleo haujafikiwa wakati mwaka wa bajeti umebaki robo tu kuisha.

Akitoa maoni jana kuhusu Mpango wa Maendeleo wa Taifa, Kiwango na Ukomo wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2017/18, Silinde alisema katika miezi tisa, Serikali imetekeleza asilimia 26 kwa kupeleka fedha za miradi ya maendeleo.

“Hawawezi kumaliza asilimia 74 zilizobaki katika kipindi cha robo mwaka kilichobaki,” alisema.

Alisema hali hiyo inatokana na sababu nyingi, ikiwamo makusanyo ya ndani ya nchi kutumika kulipa mishahara na madeni.

Silinde ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, alisema kwa mwezi Serikali imekuwa ikikusanya wastani wa  Sh1 trilioni na Sh570 bilioni hutumika kulipa mishahara ya watumishi wa umma, huku kiasi kilichobaki kikitumika kulipa madeni.