Halmashauri yanyooshewa kidole kwa kushindwa kukusanya mapato

Muktasari:

Akizungumza kwenye Baraza la Madiwani juzi, Diwani wa Kabanga, Said Mkubila alisema halmashauri hiyo imeshindwa kuwasimamia watendaji wake katika ukusanyaji  mapato licha ya kuwapo vyanzo vingi kila kijiji.

Ngara. Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera imelalamikiwa kwa kushindwa kukusanya mapato ya kutosha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza kwenye Baraza la Madiwani juzi, Diwani wa Kabanga, Said Mkubila alisema halmashauri hiyo imeshindwa kuwasimamia watendaji wake katika ukusanyaji  mapato licha ya kuwapo vyanzo vingi kila kijiji.

Akiwasilisha bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kwenye Baraza la Madiwani juzi, Ofisa Mipango wa Halmashauri hiyo, Nabigambo Amos alisema halmashauri hiyo imepokea Sh16.35 bilioni kati ya Sh36.11 bilioni zilizoidhinishwa na Serikali Kuu kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Amos alisema Sh710 milioni ni makusanyo ya vyanzo vya ndani, Sh12.14 bilioni ni mishahara na Sh774.5 milioni  ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na Sh2.7 bilioni za  miradi ya maendeleo kutoka Serikali Kuu.