Hofu ya ugaidi yatawala, Ufaransa wakimchagua Rais mpya leo

Muktasari:

Miongoni mwa wagombea hao wamo ambao wamefanya kazi  serikalini, akiwamo Emmanuel Macron,Marine le Pen na Jean-Luc Melenchon.

Paris. Raia wa Ufaransa wanatarajia kuanza kupiga kura saa chache zijazo kwa ajili ya kumpata Rais mpya wa nchi hiyo.

Wanasiasa 11 wanawania kiti cha uraisi huku wagombea wanne wakionekana kuchuana kwa umaarufu.

Miongoni mwa wagombea hao wamo ambao wamefanya kazi  serikalini, akiwamo Emmanuel Macron,Marine le Pen na Jean-Luc Melenchon.

Usalama umeimarishwa kufuatia shambulizi la kigaidi lililotokea katikati ya mji mkuu wa Paris alhamisi wiki hii, ambapo ofisa mmoja wa polisi aliuwawa.