JPM: Naujua umaskini, nimeuza maziwa na furu

Muktasari:

Rais Magufuli alisema kwamba amechunga ng’ombe na hataki asahau alipotoka na wala hapendi kuona Watanzania wanaoishi maisha ya chini wakionewa.

Chato. Rais John Magufuli, amesema ataendelea kuwatetea Watanzania maskini na wenye kipato cha chini kwa sababu hata yeye ameishi maisha duni.

Magufuli ameyasema hayo leo Jumatatu, Julai 10 wilayani Chato wakati wa uzinduzi wa nyumba 50 zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation.

“Nimeuza maziwa, nimeuza furu, nimechunga ng’ombe. Sitaki nisahahu nilipotoka, sitaki nisahau maisha ya Watanzania, sitaki Watanzania wenye maisha ya chini waonewe,” amesema.