JPM-Mafanikio ya Muungano ni juhudi za viongozi

Muktasari:

Rais Magufuli ambaye anaendelea kuhutubia katika sherehe za Muungano zinazofanyika Dodoma sasa hivi alisema Muungano huo umefanikiwa kwani mpaka sasa nchi za Unguja na Tanganyika zimetawaliwa na amani.

Dodoma. Rais John Magufuli amesema mafanikio yaliyopatikana kutokana na Muungano yamefanikishwa kutokana na juhudi za viongozi wa taifa na waasisi wa Muungano huo.

Rais Magufuli ambaye anaendelea kuhutubia katika sherehe za Muungano zinazofanyika Dodoma sasa hivi alisema Muungano huo umefanikiwa kwani mpaka sasa nchi za Unguja na Tanganyika zimetawaliwa na amani.

‘Ukiona vyaelea ujue vimeundwa, mafanikio haya yametokana na juhusi za viongozi wetu,” amesema