JPM amshukuru Zuma kwa mchango wa madawati

Picha ya mtandao

Muktasari:

Rais Magufuli ametoa shukrani hizo leo (Alhamisi) wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hiyo.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemshukuru Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini kwa mchango wa madawati uliotolewa na Serikali yake wakati wa kampeni za kuchangia madawati.

Rais Magufuli ametoa shukrani hizo leo (Alhamisi) wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hiyo.

Amesema Serikali ya Afrika Kusini ambayo imekuwa na ushirikiano mzuri na Tanzania ilikuwa miongoni mwa wachangiaji wa madawati wakati wa kampeni hiyo.

Kutokana na mchango wa madawati zaidi ya 1,000, Rais Magufuli amemshukuru Zuma akisema nchini hizo mbili zitaendelea kudumisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali.