Jafo atoa siku nne kwa Ma-Ras kumpatia takwimu

Naibu Waziri Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo

Muktasari:

Alitoa agizo hilo jana alipofungua mafunzo ya siku nne ya kuwajengea uwezo wawezeshaji wa kitaifa wa mfumo huo  yanayofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.

Morogoro. Naibu Waziri Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo ametoa siku nne kwa makatibu tawala wa mikoa (Ras) nchini kumpelekea takwimu za vituo vya afya vinavyotakiwa kufungwa mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya ukusanyaji mapato.

Alitoa agizo hilo jana alipofungua mafunzo ya siku nne ya kuwajengea uwezo wawezeshaji wa kitaifa wa mfumo huo  yanayofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.

Alisema Ras ambaye hatatekeleza agizo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Jafo alisema hadi Oktoba, vituo 65 vya afya ndivyo vilivyokuwa vimefunga mfumo wa Tehama kati ya vyote 5,511 vilivyopo nchi nzima.