Jaji Mkuu wa Kenya afunguka

Muktasari:

  • Amedai kuwa IGP Boinett amepuuzia usalama wa majaji
  • Pamoja na kutoa tuhuma hizo katika tamko la Tume ya Majaji, Maraga amesema hilo halitawarudisha nyuma katika kuilinda katiba na pia wapo tayari kulipia kwa gharama yoyote.

 Jaji Mkuu wa Kenya, David Maraga amemtuhumu Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP), Joseph Boinett kwa kupuuzia usalama wa majaji na kwamba anahatarisha maisha yao.

Pamoja na kutoa tuhuma hizo katika tamko la Tume ya Majaji, Maraga amesema hilo halitawarudisha nyuma katika kuilinda katiba na pia wapo tayari kulipia kwa gharama yoyote.

Mtandao wa Gazeti la Daily Nation unamnukuu Maraga akisema: “We are ready to pay the ultimate price for defending the Constitution and the rule of law” (Tupo tayari kulipa gharama yoyote kutetea katiba na utawala wa sheria).

Tamko hilo linamlaumu Boinett kwa kupuuzia wito wa majaji kutaka wapewe ulinzi jambo ambalo linawaweka wao na mali zao katika hatari.

Lilifafanua kuwa mahakama ni mkono wa Serikali kama Bunge na Rais hivyo wanastahili kupewa ulinzi pale wanapoona

“Kama viongozi wamechoka kuwa na mahakama imara, waitishe kura ya maoni iondolewe. Lakini kabla hilo halijafanyika, mahakama itaendelea kufanya kazi yake kama inavyostahili kwa kuzingatia katiba,” ilisisitiza taarifa hiyo