Jamhuri yagonga kisiki kesi ya Bilionea Msuya

Muktasari:

Uamuzi huo umetolewa siku moja baada ya Mahakama hiyo kutupilia mbali rufani ya washtakiwa saba katika kesi hiyo ya kupinga mahakama kupokea barua ya makabidhiano ya vielelezo vya upande wa mashtaka kwa kuwa washtakiwa hawajatiwa hatiani katika shtaka hilo, hivyo si sahihi kukatia rufani uamuzi wa awali katika shauri hilo.

Arusha. Mahakama ya Rufaa jana ilitupilia mbali rufani ya Jamhuri  katika kesi ya mauaji ya bilionea Erasto Msuya kutaka kupokelewa ushahidi wa kielelezo cha gari la aina ya Range Rover lililokuwa likiendeshwa na marehemu.

Uamuzi huo umetolewa siku moja baada ya Mahakama hiyo kutupilia mbali rufani ya washtakiwa saba katika kesi hiyo ya kupinga mahakama kupokea barua ya makabidhiano ya vielelezo vya upande wa mashtaka kwa kuwa washtakiwa hawajatiwa hatiani katika shtaka hilo, hivyo si sahihi kukatia rufani uamuzi wa awali katika shauri hilo.

Katika shauri la jana, shahidi wa tisa katika kesi hiyo, Inspekta Samweli Maimu alitaka kuwasilisha gari hilo kama sehemu ya kielelezo katika kesi hiyo, inayowakabili watu saba.

Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Eddie Fussi akisoma uamuzi wa majaji watatu wa mahakama ya hiyo; Edward Rutakangwa, Angela Kileo na Salum Masati alisema w