Jukwaa la wahariri laishukia CUF

Katibu wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Neville Meena

Muktasari:

Akizungumza na wanahabari leo, Katibu wa Jukwaa hilo, Neville Meena amesema si salama wafuasi wa chama kujaa kwenye vyumba vya mikutano.

Dar es Salaam. Jukwaa la Wahariri nchini (TEF) limelaani kitendo cha waandishi wa habari kujeruhiwa katika tukio la uvamizi lililotokea katika mkutano wa CUF hivi karibuni.

Akizungumza na wanahabari leo, Katibu wa Jukwaa hilo, Neville Meena amesema si salama wafuasi wa chama kujaa kwenye vyumba vya mikutano.

“CUF wajue kwa mara nyingine wapo  kuwa kwenye uangalizi tunawatazama, uamuzi unaweza kuwa wakati wowote kwa sababu tunatakiwa kuhakikisha watu wetu wapo salama,” amesema

Meena alilaani pia tabia ya baadhi ya viongozi wa CUF kuwapangia waandishi habari za kuandika.

“Ni wajibu wetu kusikiliza kila upande, habari ya kupangiwa cha kufanya au upande wa kuripoti sio la kwetu, kuna wanaodhani wanajua habari kuliko sisi tuliosomea.” amesema