Kansela Merkel akwama kuunda serikali

Muktasari:

Kutokana na hali hiyo Kansela Merkel amewaambia waandishi wa habari kuwa atamwarifu Rais wa Shirikisho kuhusu kuvunjika kwa mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto wa vyama.

Merkel alilazimika kufanya mazungumzo na vyama vingine baada ya kukosa wingi wa kura za kukiwezesha chama chake kuunda serikali. Lakini baada ya mazungumzo ya siku kadhaa na chama cha FDP kinachopendelea wafanyabiashara, kiongozi wake Christian Lindner aliamua kujiondoa akisema “hakukuwa na msingi wa kuaminiana” kuunda serikali na muungano wa wahafidhna wa CDU-CSU na wana mazingira.

Berlin, Ujerumani. Kansela Angela Merkel jana aliachwa akifikiria hali ya baadaye kisiasa baada ya mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto kuvunjika na kuiingiza Ujerumani katika mkwamo wa kisiasa unaoweza kulazimisha kufanyika uchaguzi mpya wa mapema.

Mazungumzo hayo yalikuwa yanahusisha chama tawala cha Christian Democratic Union (CDU na chama ndugu cha SCU) kinachoongozwa na Merkel pamoja na Free Democratic (FDP) na cha Watetezi wa Mazingira linzi wa (Die Grüne), lakini yalivunjika baada ya chama cha FDP.

Kutokana na hali hiyo Kansela Merkel amewaambia waandishi wa habari kuwa atamwarifu Rais wa Shirikisho kuhusu kuvunjika kwa mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto wa vyama.

Merkel alilazimika kufanya mazungumzo na vyama vingine baada ya kukosa wingi wa kura za kukiwezesha chama chake kuunda serikali. Lakini baada ya mazungumzo ya siku kadhaa na chama cha FDP kinachopendelea wafanyabiashara, kiongozi wake Christian Lindner aliamua kujiondoa akisema “hakukuwa na msingi wa kuaminiana” kuunda serikali na muungano wa wahafidhna wa CDU-CSU na wana mazingira.

"Ni bora kutoongoza kuliko kuongoza vibaya," alisema Lindner na akaongeza kwamba vyama havikuwa na “dira ya pamoja juu ya kuiboresha" Ujerumani.

Akionyesha masikitiko yake, Merkel ameapa kuipitisha salama Ujerumani katika kipindi kigumu cha mkwamo wa kisiasa.

Ujerumani, taifa lenye uchumi mkubwa barani Ulaya, sasa inakabiliwa na wiki kadhaa, kama si miezi ya mkwamo huku serikali ikiwa haina uwezo wa kupitisha sera muhimu.

"Mimi kama kansela...Nitafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa nchi hii inajikwamua katika kipindi hiki kigumu,” alisema.