Kenya yasema haina fedha za kuwalipa madaktari waliogoma

Muktasari:

Madaktari wa Kenya walianza mgomo wakishinikizwa kuongezwa mishahara kuanzia Desemba mwaka jana na baadaye Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyata aliomba madaktari 500 kutoka Tanzania wakafanye kazi Kenya.

Nairobi. Serikali ya Kenya imesema haina fedha za kuwalipa mishahara ya miezi mitatu madaktari waliogoma.

Madaktari wa Kenya walianza mgomo wakishinikizwa kuongezwa mishahara kuanzia Desemba mwaka jana na baadaye Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyata aliomba madaktari 500 kutoka Tanzania wakafanye kazi Kenya.

Lakini hivi karibuni madaktari hao walitangaza kurudi kazini lakini wakataka walipwe mishahara ya miezi mitatu waliyogoma. Rais Kenyata aliridhia madaktari hao kulipwa mishahara hiyo.

Mwenyekiti wa Baraza la Magavana, Peter Munya alisema serikali haina shida kuwalipa mishahara na marupurupu madaktari hao lakini tatizo ni kuwa hakuna fedha.