Kero ya maji Mugumu kutatuliwa

Muktasari:

Mji huo unaokadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya 75,000, kuanzia Mei, hadi sasa unakabiliwa na tatizo la maji linalosababisha kuongezeka gharama za maisha.

Serengeti. Wizara ya Maji na Umwagiliaji imeahidi kutatua tatizo la ukosefu wa maji kwenye Mji wa Mugumu wilayani hapa, kwa kutoa pampu kutokana na zilizokuwapo kuungua mara tatu katika kipindi cha miezi mitano.

Mji huo unaokadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya 75,000, kuanzia Mei, hadi sasa unakabiliwa na tatizo la maji linalosababisha kuongezeka gharama za maisha.

Mbunge wa Serengeti, Marwa Ryoba alisema wizara hiyo imeahidi kutuma wataalamu kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo kwa sababu linajirudia.