Kesi ya Lissu yapigwa kalenda

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa kesi hiyo ambayo ipo katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfey Mwambapa imeahirishwa kwa sababu yupo likizo.
  • Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anadaiwa kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Dar es Salaam.  Kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirishwa hadi Aprili 3, mwaka huu.

Kwa mujibu wa kesi hiyo ambayo ipo katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfey Mwambapa imeahirishwa kwa sababu yupo likizo.

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anadaiwa kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Anadaiwa kuwa Juni 28, mwaka huu, Lissu akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alitoa kauli za uchochezi kuwa:“Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidiktekta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote, huyu dikitekta uchwara lazima apingwe kila sehemu. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene.’’