Kibiti shwari, anayetaka na aende – ACP Mwakalukwa

Msemaji wa Jeshi la Polisi, kamishina msaidizi wa Polisi (ACP), Barnabas Mwakalukwa

Muktasari:

Ameyasema haya wakati akizungumza na wahariri wa Mwananchi Communications Limited (MCL) alipofanya ziara ya kujionea shughuli za kampuni hiyo.

Dar es Salaam. Msemaji wa Jeshi la Polisi, kamishina msaidizi wa Polisi (ACP), Barnabas Mwakalukwa, amesema hali ya usalama katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji imeimarika sana na watanzania wanaweza kwendsa huko kufanya shughuli zao buila woga.

Ameyasema haya wakati akizungumza na wahariri wa Mwananchi Communications Limited (MCL) alipofanya ziara ya kujionea shughuli za kampuni hiyo.

ACP Mwakalukwa amesema tangu kuanzishwa kwa kanda maalum ya polisi katika eneo hilo, matukio ya uhalifu yamepungua na polisi wameweza kwa kiasi kikubwa kuwadhibiti watu waliokuwa wanafanya uhalifu.

Hata hivyo, ameviomba vyombo vya habari na waandishi nchini kusaidia kusambaza taarifa hizo ili kurudisha Imani ya wananchi.

“Zile taarifa kuwa sasa hivi eka 3,000 za ardhi Kibiti zinauzwa sh1,000 na hakuna mtu anayekwenda si za kweli. Hivi sasa hali ni shwaari Kibiti ana anayetaka kwenda anede… hata mimi nitakwenda huko,” amesema na kuongezaa:

“Mimi Nina mpngo wa kwenda kibiti bila vyombo vya habari… Andikeni habari nzuri za Kibiti, Hata nikitoka Leo muandike Kibiti shwari.”